Watu wenye ulemavu wametakiwa kutumia fursa ya kupewa viungo vya bandia ili kufanya shughuli zao za kuwaletea maendeleo na kuawainua kiuchumi kiurahisi
Hayo yamesemwa leo tarehe 19/2 /2021 na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu Ummy Nderiananga katika Ukumbi wa Orofea uliopo Manispaa ya Iringa ambapo alikuwa mgeni rasmi katika shughuli ya ugawaji wa viungo vya bandia
Mh.Nderiananga amesisutiza kuwa walemavu siyo watu wadhaifu bali wana uwezo wa kufanya shughuli yeyote kwa ufanisi kama watu wengine hivyo kuwashukuru kampuni ya Kamal ambayo imewapa walemavu wa Manispaa vifaa bila gharama yeyote vifaa hivyo vimewapa ujasiri zaidi wa kuweza kufanya shughuli zao bila hofu yeyote na kwa ufanisi hivyo kuwaongezea kipato na kutegemewa katika familia na jamii kwa ujumla
Aidha waziri ameishukuru kampuni ya Kamal kwa moyo wa upendo waliouonyesha na kurudisha matumaini yaliyopotea kwa walemavu hao
Pia amemshukuru Mhe.Mstahiki Meya Manispaa kwa mikakati mizuri alinayo juu ya walemavu.
Mwakilishi wa chama cha mapinduzi Mkoa katibu Said Kaduro amewataka walemavu kutokukata tamaa badala yake kuwa wajasiri katika kutafuta maendeleo kwani uwezo na nguvu wanazo.
Pia anawashukuru Mbunge na Mstahiki Meya pamoja na watendaji wote kwa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi
Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa mhe.Ibrahim Ngwada amesema ataendelea kuunga mkono jitihada za wadau wanaotaka kutoa Misaada kwa watu wenye ulemavu ili kuhakikisha wanafanya hivyo bila kupata vikwazo
Mh. Rita Kabati Mbunge viti maalum Mkoa wa Iringa amesema anatambua na kuthamini jitihada zilizofanywa na timu ya madaktari kutoka kampuni ya Kamal kwa moyo wao wa kipekee kwa huduma nzuri ya kuwapima mpaka kuwapatia viungo vya bandia ambavyo vitarahisisha maisha na utendaji kazi wa watu wenye ulemavu Zaidi ya 51
Mh.Rita amekemea tabia ya baadhi ya watu kuwatumia walemavu kama kitega uchumi amesema jambo hilo halileti afya katika jamii yetu
Aidha mh.Kabati amemuomba Naibu waziri kuangalia namna ya kuwasaidia kinamama wanaojifungua watoto wenye ulemavu kwani mara nyingi waume zao huwanyenyepaa na kuwakimbia hivyo kujikuta katika wakati mgumu wa kulea watoto hao peke yao
Kampuni ya Kamal ya Jijini Dar es Salaam inajihusisha na kutengeneza vifaa vya bandia kwa walemavu Nchini Tanzania tayari wamekwishatoa vifaa zaidi ya 3500 na wanatarajia kugawa vifaa 2500 kwa kipindi hiki na kwa Manispaa ya Iringa wametoa vifaa 51 na kuwapima walemavu 32
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa