Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mheshimiwa Capt.George Mkuchika amewaasa watumishi wa Manispaa ya Iringa, Halmashauri ya wilaya ya Iringa pamoja na Taasisi mbalimbali za serikali zilizopo Mkoa wa Iringa kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Mheshimiwa Mkuchika ametoa kauli hiyo katika kikao kazi cha watumishi wa uma waliopo mkoa wa Iringa kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni kiliomo ambapo apia amewataka watumishi kutii maadili ya kazi katikia kuwahudumia wananchi
Aidha amesisitiza kuwa Serikali inazingatia suala la uhamisho kwa watumishi wote kwani uhamisho ni haki ya mtumishi yeyote ili mradi taratibu zifuatwe katika kutekeleza.
Amezipongeza pia juhudi zinazofanywa na serikali kwa kulipa madeni ya walimu na kuendelea kuhakiki ambao hawajalipwa ili wapatiwe fedha zao akiitaja kuwa ni juhudi kubwa katika serikali ya awamu ya tano.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Mkurugenzi wa Wilaya ya Iringa, Meya wa Manispaa, Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa ,Kaimu katibu Tawala, kamati ya ulinzi, wakurugenzi, Tarura, Takukuru, Tanroad, Nssf , Mkurabita , na Tasaf.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa