Mwenyekiti wa kamati ya Ushauri Wilaya ambaye ndiye Mkuu wa Wilaya ya halmashauri ya manispaa Iringa Mhe. Veronica Kessy amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka shule watoto wao na kuanzia tarehe 1/02/2024 msako mkali utaanza nyumba hadi nyumba kuwabaini wazazi na walezi ambao watoto wao hawajaripoti shuleni na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Veronica Kessy amaetamka maneno hayo katika kikao cha Kamati na Ushauri Wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa na Kilimo siku ya Jumatano tarehe 25/01/2024.
Aidha alitoa rai kwa wajumbe na watu wa afya kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa kipindupindu na wafikishe elimu kuanzia ngazi ya familia mpaka kwenye jamii inayowazunguka.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa