MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini Dkt.Jesca Msambatavangu amewataka wazazi na walezi kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekwa vikiripotiwa kuongezeka siku hadi siku katika baadhi ya maeneo Manispaa ya Iringa.
Msambatavangu ameyasema hayo Julai 8 2023. Katika Kata ya Nduli Mtaa wa Msisina na Mtalagala wakati akihitimisha ziara yake ya Siku 8 iliyofanyika Mtaa kwa Mtaa ,Kata kwa Kata kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, huku akiwaeleza namna ambavyo Serikali ya awamu ya sita ilivyotoa zaidi ya shs.bilioni 39 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Sekta ya Elimu,Afya na miundombinu Katika Halimashauri.
Msambatavangu amesema kumekuwa na Wimbi la vitendo vya ukatili wanaofanyiwa watoto kama ubakaji na ulawiti hivyo amewaasa wazazi na Walezi kuwa makini kuhakikisha wanawalinda watoto wasifanyiwe vitendo hivyo kwani vinaathiri afya ya mwili, akili na kumfanya mtoto kukosa ujasiri.
'Nawaomba sana walindeni watoto wapeni haki zote za msingi kwani mkiwatendea mema watoto hawa mmemtendea Mungu na atawabariki,mkitaka laana basi watendeeni watoto hawa mabaya alisema Msambatavangu.'
Kwa upande wa utekelezaji wa miradi ya Maendeleo Dkt.Jesca amesema katka kipindi cha mwaka 2021 hadi Juni 2023 Miradi mingi ya Maendeleo imetekelezwa na Halmashauri kutokana na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kumwaga fedha nyingi katika ili kuwasogezea karibu wananchi huduma za vituo vya afya,zahanati,madarasa na kuboresha miundo mbunu ya barabara .
Awali Diwani wa Kata ya Nduli Mhe.Bashiri Mtove amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za Miradi mbali mbali ya aendeleo ambapo Kata ya Nduli imenufaika na fedha hizo kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nduli,zahanati ya Mtalagala na Barabara ya Mgongo-msisina na upanuzi wa uwanja wa Ndege Nduli ambao uko hatua ya ukamilishaji.
Wakitoa kero na changamoto zao wananchi wa Msisina na Mtalagala wamesema kero kubwa ni ukosefu wa maji,umeme na ukosefu wa shule ya Sekondari hivyo kupelekea wanafunzi kutembea umbali mrefu kufika shuleni.
Akijibu kero hizo Mbunge amesema kuhusu Shule eneo limepattikana hivyo waanze utaratibu wa ujenzi kwa kushirikiana na ofisi ya Kata huku akiahidi kutafuta ufumbuzi changamoto ya maji na umeme.
Ziara ya Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini iliyoanza Julai 1 2023 imemalizika leo Julai 8 2023 ambapo iliwashirikisha viongozi mbali mbali wa chama na Serikali.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa