Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMi) Selemani Jafo amesema ameridhishwa na ujenzi wa mradi wa Stendi ya Igumbilo awamu ya pili jengo la abiria, choo pamoja na Kituo cha Polisi na kuwapongeza viongozi wa Halmashauri ya Manispaa na Mkoa kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.
Jafo ameyasema hayo leo tarehe 21/12/2020 kwenye ziara ya siku moja ambapo ametembelea na kukagua mradi huo na amewataka viongozi kujifunza kutoka Halmashauri zingine ambazo zimefanya vizuri zaidi katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao pia amesisitiza Halmashauri zitumie mapato yake ya ndani katika kuwekeza miradi kuongezea Halmashauri mapato.
Afisa Mipango wa Manispaa ya Iringa Herbet Bilia akisoma taarifa ya mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi, amesema mradi mpaka sasa umegharimu kiasi cha Tsh 1.4 billion na kuwa pindi utakapoanza kazi utaiingizia Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kiasi cha Tsh milioni 500 kwa mwaka.
Ziara hiyo imewashirikisha Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini mhe. Jesca Msambatavangu, Mbunge wa vitimaalum Mkoa wa Iringa Mhe.Ritta Kabati, Mkuu wa wilaya ya Iringa ndugu Richard Kasesela, Katibu Tawala Mkoa ndugu Happiness Seneda, wakuu wa Idara na vitengo Manispaa na Mkoa wa Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa