Mh.Lukuvi ameyasema hayo kwenye uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya wakati akifungua rasmi maonesho ya nane nane kanda ya nyanda za juu kusini na kutembelea baadhi ya mabanda yaliyopo eneo hilo.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ndugu Albert chalamila amewataka wananchi kutumia vizuri haki yao ya msingi ya kikatiba kuchagua viongozi bora kwa maendeleo ya kilimo,mifugo na Uvuvi kama kauli mbiu ya maonesho ya nane mwaka huu inavyosema.
Maonesho hayo yamefunguliwa leo rasmi na mgeni rasmi alikuwa Mh Wiliam Lukuvi ambaye aliongozana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali akiwemo Naibu spika wa binge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,Mh.Tulia Akson na yanatarajiwa kufungwa tarehe 8/8) mwaka huu na Mh.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa