“Nimeridhika na kufurahishwa na utendaji Kazi wa Watumishi wa Mkoa wa Iringa na sijaona dosari yoyote katika Manispaa hizi, niwapongeze Watendaji na Mkuu wa Mkoa kwa kusimamia Miradi mingi ya Maendeleo, inaonekana mna ushirikiano sana endeleeni kuwa na Mahusiano mazuri ili Halmashauri zetu ziweze kusonga mbele.”
Kauli hiyo imesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa katika Ukumbi wa Kichangani tarehe 28/9/2019 katika Ziara yake Mkoani Iringa alipokuwa akiongea na Watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Mbali na hayo amesema kuwa Serikali yetu inaheshimu na kuthamini Kazi wanazozifanya, nyie ni Watumishi wa Umma ni vizuri kutambua kuwa bila Wananchi tusingekuwa hapa, amesisitiza watumishi wasiwe wakaaji wa Maofisini wawe wanawatembelea Wananchi na kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa