“Serikali ya awamu ya tano inaendelea kupambana na watu wanaojihusisha na usafirishaji, uuzaji na matumizi ya madawa ya kulevya" haya yamesemwa na Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Kassim Majaliwa katika maadhimisho ya siku ya kupambana na madawa ya kulevya ambapo Kitaifa yamefanyika Mkoani Iringa katika viwanja vya Kichangani.
Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Iringa katika maadhimisho haya Mh.Waziri amewaasa kuacha kutumia dawa za kulevya kwani hupunguza uwezo kazi katika Taifa letu hasa kipindi hiki cha kasi ya viwanda
Aina ya madawa ya kulevya yanapatikana kwa uraisi ni Bangi, Heroine na Cocaine ambapo hupelekea kudorora kwa nguvu kazi ya taifa hasa kwa vijana wa jinsia zote wenye umri kuanzia miaka kumi na tano hadi miaka arobaini na tano.
Aidha maadhimisho yaliongozwa na Kauli mbiu isemayo TUJENGE MAISHA YETU, JAMII YETU NA UTU WETU BILA MADAWA ZA KULEVYA
Mh. Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Iringa kwa maandalizi haya ya maadhimisho ya kupamabana na madawa ya kulevya .
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa