Katika kutekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda Waziri wa Nishati Mh, DKT. Medard Kalemani ameendesha Washa fupi ya kujenga Mradi wa uzalishaji wa umeme kupitia nishati ya maji (Rufiji Hydropawer project) iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni kilimo Manispaa ya Iringa
Katika warsha hiyo Mh Kalemani amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Iringa kusimamia Sheria za Mazingira ili kutunza vyanzo vya maji ya Mto Rauha ambapo mradi utapita na kusaidia ongezeko la maji pamoja na kutunza uhalisia wa mazingira
Aidha akieleza faida za Mradi huo Mh Waziri amesema kuwa Mradi ukikamilika utasaidi uzalishaji wa Megawat 2,100 ambazo pia zitasaidia katika ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha pawer housed chenye uwezo wa kuzalisha megawati 235,kitakachosaidia kupunguza gharama za Umeme pamoja na kuongezeka kwa uwekezaji katika Viwanda.
Mradi huo unatarajia kukamilika katika kipindi cha miezi 39 ikiwemo miezi 3 ya ufungaji wa mitambo ya kuzalishia Umeme na kuendeleza mradi wa umeme vijijini (REA) Hivyo utaleta Ukombozi kwa Wajasiriamali wadogo wadogo wenye lengo la kuanzisha Viwanda vya kusindika
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa