Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada ametoa wito kwa wenyeviti wote wa Serikali za mitaa Manispaa ya Iringa kuwalinda watoto na ukatili wa kijinsia kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza wimbi la matukio ya ulawiti na ubakaji ndani ya Manispaa yetu
Hayo yamesemwa leo tarehe 12/01/2021, katika ukumbi wa Orofea ambapo Mhe. Ngwada alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo ya siku tatu ya ulinzi na usalama wa mtoto kwa wenyeviti hao
Mhe. Ngwada amesema kesi nyingi za ukatili mara nyingi zinaishia kwenye mitaa kwani wahusika wa vitendo hivyo ni kama majirani, ndugu wa karibu au marafiki wa karibu wa waathirika wa ukatili hivyo amewataka wenyeviti kutokuyafumbia macho matukio hayo bali kuwajibika kikamilifu kuhakikisha wanamaliza kabisa tatizo hilo katika mitaa yao
Nae Mwenyekiti wa Umoja wa vijaja CCM Wilaya ndugu Salvatory Ngelela amesema ustawi wa vijana katika jamii unategemema sana usalama wa watoto hivyo kuitaka jamii kuwalinda watoto waweze kutimiza ndoto zao
Tinieli Mbaga ni Afisa ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa awali akimkaribisha mgeni rasmi amesema lengo la mafunzo hayo kwa wenyeviti wa mitaa ni kuwajengea uwezo ili waweze kudhibiti wimbi la vitendo hivyo viovu ambavyo vimekuwa vikishamiri siku hadi siku dhidi ya watoto wetu
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Gangilonga Dr. Mengele ameshukuru kupata mafunzo hayo kwani yatawasaidia kupambana na matukio ya aina hiyo na kuwa hawako tayari kuyafumbia macho katika mitaa yao watahakikisha sheria inafata mkondo wake dhidi ya watuhumiwa watakaobainika
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa