Mbunge wa Iringa mjini Mh. Jesca Msambatavangu ameahidi kutoa elimu bure ya wajasiriamali ndani ya Manispaa itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi
Hayo ameyaahidi leo tarehe 15/12/2020, katika kongamano la elimu kwa vikundi vya wajasiriamali Manispaa ya Iringa lililofanyika katika ukumbi wa Kichangani, likiwa limeandaliwa chini ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kupitia Ofisi ya Maendeleo ya Jamii
Mhe. Jesca ameendelea kuwaambia wajasiriamali hao kuwa Iringa inafursa nyingi hasa katika sekta ya kilimo hivyo na wao wasisite kulima maana kilimo ni uti wa mgongo kwa Taifa letu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesera akiwa ameambatana na Mbuge nae amewataka wajasiriamali hao kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwani kupitia wataalamu hao, wengi wamefanikiwa kukua kiuchumi.
"Fanya hayo yote ila usipomcha Mungu hutaambulia kitu maana yeye ndie mtoa vyote, vivyo hivyo wajasiriamali mjitahidi kutumia fursa mbalimbali za kimaisha katika kujiongezea kipato " Kasesera aliongezea hayo kama sehemu ya hamasa kwa washiriki waliohudhuria mafunzo
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndugu. Hamid Njovu amewataka wajasiriamali hao kubadilisha mtazamo wa maisha katika biashara zao, sambamba na hilo amegawa vyeti kwa wadau mbalimbali wanaoshirikiana kikamilifu katika shughuli za ujasiriamali ndani ya Manispaa.
Mwantumu Dosi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Iringa amewataka viongozi wa makundi hayo ya wajasiriamali kujitahidi kusimamia namna ya utumiaji wa mikopo wanayopatiwa pamoja na shughuli wanazozifanya ili zilete tija kwao.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa