Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bi. Tupe Kayinga amewaongoza walimu, wananchi na wanafunzi katika zoezi la upandaji wa Miti ya vivuli na Matunda katika Shule mpya ya Sekondari Kwavava iliyopo Kata ya Kitwiru.
Kayinga amewaelekeza wanafunzi kuitunza miti hiyo ili iweze kustawi na kusema kila mwanafunzi atakapomaliza shule anatakiwa aonyeshe miti aliyoipanda wakati akiwa shuleni hapo (Graduate with a Tree).
Kayinga amewashukuru Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kutoa Miche 2000 ambapo leo imepandwa miche 1500 na kusema kuwa zoezi hilo la upandaji miti ni endelevu.
Ndg.Lucas Bwire ni Mhifadhi Misitu na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Mkoani Iringa amesema wamekuwa wakigawa miche mbalimbali ya Matunda na vivuli kwenye Taasisi mbalimbali na kwa wananchi bure kwa lengo la kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo ametoa wito kwa wenye uhitaji wa miche wawasiliane nao kwani bado wanaendelea na ugawaji wa miche kwa wanaohitaji.
Aidha amemshukuru Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuIona Kata ya Kitwiru na kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ambayo imeondoa changamoto ya wanafunzi waliokuwa wakitembea umbali mrefu wa km 18 kila siku kwenda shule ya Sekondari Ipogolo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa