Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amewataka wazazi na walezi wenye watoto wenye umri wa chini ya miaka mi 5 kujitokeza kuwapatia watoto wao chanjo ya polio.
Dendego ameyasema hayo leo tarehe 9/9/2022 wakati akizindua kampeni ya chanjo ya Polio ki Mkoa iliyofanyika Manispaa ya Iringa kata ya Kihesa
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema, kuna umuhimu mkubwa wa wazazi kuwapatia watoto wao chanjo hiyo ili kuwaepusha na madhara yatakayowapata endapo wakikosa chanjo hiyo ikiwemo ulemavu au kupoteza maisha kwa watoto wao
Na kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa ambaye ni Diwani wa Kata ya Kihesa Mhe. Juli Sawani amempongeza Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa zoezi hilo na amesema kuwa katika Kata yake atahakikisha watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano 5 walioko kwenye eneo lake wanapatiwa chanjo ya polio
Mohamedi Musa ni Mganga Mkuu wa Mkoa amesema zoezi hilo ni awamu ya tatu na kwa awamu ya pili zoezi hilo lililkuwa na mafanikio mkubwa hadi kuvuka malengo ya asilimia 116 ya uchanjaji huku kwa sasa wakitarajia kuwafikia watoto zaidi ya laki mbili (200,000)
Hata hivyo Bi. Getrude Mlawa ambaye amejitokeza kumpatia mtoto wake chanjo hiyo amesema anaamini chanjo ni salama na amewataka wazazi wengine kuwatoa watoto wao ndani ili waweze kupatiwa chanjo hiyo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa