Kamati ya kudhibiti Ukimwi ya Manispaa ya Iringa chini ya Mwenyeti wake Naibu Meya Mheshimiwa Nzala Ryata imefanya Ziara ya kutembelea na kukagua kikundi cha Kijamii kinachojishughulisha na Ufugaji na Ujasiliamali kilichopo kata ya Kitwiru. Kikundi kilipata Mchango wa Shilingi Milioni moja kutoka Manispaa ya Iringa lengo likiwa ni kuongeza mtaji wa Ufugaji
Aidha Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe Nzala Ryata amewaomba wanakikundi cha Twisuka kuzingatia matumizi sahihi ya dawa na kuacha au kupunguza kabisa Ngono Zembe na kusimamia vizuri Kikundi na Miradi yake ili Wanachama waweze kujikwamua Kiuchumi
Pia Kamati imetembelea Shule ya Sekondari ya Mtwivila ilikuweza kuona ni jinsi gani Wanafunzi wanapata Elimu ya Ugonjwa wa Ukimwi kupitia Taasisi mbalimbali
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa