“ Wakuu wa wilaya na wakurugenzi wote ndani ya mkoa wa Iringa hakikisheni mnasimamia watumishi walio chini yenu na tengeni muda wenu kusimamia miradi ya maendeleo katika wilaya zenu.”
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa Mheshimiwa Ally Hapi alipokuwa akihutubia wananchi wa mkoa wa Iringa katika mkutano wa majumuisho wa ziara ya IRINGA MPYA katika viwanja vya mwembetogwa Manispaa ya Iringa.
Katika Manispaa ya Iringa ziara ya mkuu wa mkoa ilianza tarehe26/9/2018 mpaka tarehe 29/9/2018 ambapo jumla ya miradi sita ya maendeleo ilitembelewa na mkuu huyo wa mkoa ukiwemo mradi wa machinjio ya kisasa ya ngelewala, mradi wa kuzindua jengo la kufulia nguo hospitali ya frelimo, mradi wa ujenzi wa madarasa 4 shule ya msingi viziwi, mradi wa ujenzi wa bweni shule ya sekondari ya wasichana Iringa, mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi Igumbilo na mradi wa ujenzi wa madarasa mawli shule ya msingi Kigonzile.
Aidha, mradi wa ujenzi wa madarasa manne shule ya msingi viziwi ulizinduliwa na mradi wa ujenzi wa bweni shule ya sekondari ya wasichana Iringa uliwekewa jiwe la msingi. Pia mradi wa ujenzi wa jengo la kufulia katika hospitali ya frelimo ulizinduliwa.
Katika Manispaa ya Iringa mkuu wa mkoa Mheshimiwa Ally Hapi alifanya mikutano mikubwa ya kusikiliza kero za wananchi minne na mikutano midogo ya kuwafuata wananchi na kusikiliza kero zao minne ambapo jumla kwa Manispaa alifanya mikutano nane.
Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa alisikiliza na kutatua kero za wananchi ambazo zaidi zilikuwa ni kero ya ardhi, mipangomiji, afya na sheria.
Lengo la ziara ya Iringa Mpya ni kuwakumbusha watumishi wajibu wao wa kuwafuata wananchi huko chini waliko na kutatua kero zao, ambapo ameahidi kurudi tena kwenye wilaya za mkoa wa Iringa na kufuatilia maagizo yote na kero alizozipokea kama zimefanyiwa kazi
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa