Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Nicholaus Mwakasungula amewataka wauguzi wa Manispaa ya Iringa kufanya kazi kwa weledi kulingana na taaluma yao.
Ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Hospital ya wilaya ya Frelimo siku ya ijumaa tarehe 17.05. 2024.
Akihutubia wauguzi mahali hapo pia amewataka wauguzi kutoa huduma kwa wananchi kutokana na mahitaji yao huku wakizingatia uvumilivu na matendo ya huruma kwa wagonjwa.
“Naomba niwapongeze sana kwa kuandaa shughuli hii maalumu mnayofanya katika siku ya leo, lakini vilevile nawaomba mumuenzi muuguzi mwanzilishi, Bi Florance Nightngale kutokana na kujitoa kwake pamoja na utendaji wake wa kazi uliotukuka, muige mfano wake. Pia zingatieni majukumu ya kazi kwa mujibu wa taaluma yenu.”
Amesema Mwakasungula.
Naye, Muuguzi Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya iringa Bi. Afla Mtuya amewashukuru wote waliohudhuria katika tukio hilo muhimu kama ishara ya kuwakumbusha wajibu na majukumu yao katika kusimamia huduma wanazozitoa kwa wagonjwa.
Aidha, Mwakasungula ameahidi kufikisha kero na changamoto mbalimbali za wauguzi hao kwa uongozi wa Manispaa ikiwemo
upungufu wa watumishi, urekebishaji wa mishahara, vyeo kwa watumishi na upungufu wa magari maalumu ya wagonjwa (Ambulance) na vitendea kazi vinginevyo mahali pa kazi.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na wauguzi wa vituo vya afya, zahanati pamoja na Hospitali zote za Manispaa ya Iringa huku yakiongozwa kwa kauli mbiu isemayo, “Wauguzi Sauti Inayoongoza, Wekeza Katika Uuguzi, Heshimu haki, Linda afya.” Ambapo hufanyika duniani kote kila mwaka ifikapo Mei 12.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa