Ikiwa ni siku ya kwanza ya zoezi la Sensa ya watu na makazi Mratibu wa Sensa Manispaa ya Iringa ndugu Reymond Nyenza amesema Wamefakiwa kuhesabu watu katika nyumba za kulala wageni na,makundi maalum ya watoto wa mitaani kwa asilimia sabini 70.
Nyenza ameyasema hayo leo tarehe 23/8/2022 majira ya saa 7.00 usiku walipokuwa wakitimiza wajibu wa kuhesabu watu wate waliolala kwenye nyumba za kulala wageni zilizopo Manispaa ya Iringa.
Aidha Nyenza amewashukuru wahudumu na wamiliki wa Hoteli kwa ushirikiano waliouonyesha na wamefanya kazi hiyo bila usumbufu wowote.
Kwa upande wa makundi maalum pia amesema wameshirikiana na watendaji wa Kata na mitaa kuhakikisha wanapata idadi kamili ya watoto na vijana wanaolala mitaani ili kujua idadi yao na kuweza kusaidia katika kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Sensa ya watu na makazi hufanyilka kila baada ya miaka kumi na kwa mwaka huu wa 2022 inafanyika tarehe 23 Agosti Tanzania Nzima.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa