• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Environment and Cleaning
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Kazi
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma ya elimu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba

TASAF

Start Date: 2001-01-07
End Date: 2017-01-07

2.0 TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA TASAF 

Mradi wa TASAF kitaifa ulianza kutekelezwa kuanzia mwaka 2001-2005 kwa awamu ya kwanza, awamu ya pili mwaka 2006-2009 na awamu ya tatu imeanza kutekelezwa mwaka 2012 mpaka sasa. Taarifa za utekelezaji kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inaoneshwa katika maelezo hapa chini

2.1 TASAF AWAMU YA - I

Katika utekelezaji wa Mradi wa TASAF awamu ya I (2001-2005), Halmashauri ya Manispaa ya Iringa haikupata nafasi ya kutekeleza mradi huu. Sababu kubwa ilikuwa ni muongozo wa utekelezaji wa mradi ulielekezwa katika ngazi za Halmashauri za Wilaya tu.

 

2.2 TASAF AWAMU YA - II

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni mojawapo ya Halmashauri zilizopata Ufadhili kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF II) kuanzia mwaka 2006 hadi 2009. Katika kipindi hiki Halmashauri ilipokea jumla ya Tshs. 1,515,432,211 kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa madarasa 44, Maabara 1, matundu ya vyoo 116, Zahanati 2, ukarabati wa barabara 8, Vikundi 10 vya ufugaji wa kuku na nguruwe na mradi wa Mwitikio wa Jamii Dhidi ya UKIMWI (MJADU) ambao ulitekelezwa kwa mitaa 17. 

2.3 MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI TASAF - III



TASAF awamu ya III ilizinduliwa rasmi na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete mwezi Agosti, 2012 Mkoani Dodoma na utekelezaji wake ulianza kwa baadhi ya Halmashauri. Mpaka sasa Mpango huu wa Kunusuru Kaya Masikini unatekelezwa kwa Halmashauri 161 ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ulizinduliwa rasmi tarehe 06/01/2015 katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa. Uzinduzi huo ulijumuisha viongozi kutoka ngazi ya Mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Waheshimiwa Madiwani wa Kata zote, Afisa Tarafa, Wakuu wa Idara na Vitengo, wataalam kutoka Idara mbalimbali waliochaguliwa kuwa wawezeshaji ngazi ya Wilaya.

Katika Mpango huu wa Kunusuru Kaya Masikini jumla ya Mitaa 98 imefikiwa kati ya mitaa 192 iliyopo Manispaa ya Iringa. Jumla ya Kaya 2953 ndizo zinazohudumiwa na Mpango wa kunusuru Kaya masikini zenye jumla ya wanafunzi wa sekondari 616, wanafunzi wa shule ya msingi 2,031 na watoto wa kliniki 394 ambao hupata huduma katika shule za msingi 43, sekondari 12, zahanati 9 na vituo vya afya 4.

 

2.4 MADHUMUNI YA MPANGO WA TASAF - III 

Madhumuni ya TASAF awamu ya III ya Mpango wa Kunusuru Kaya ni kutoa ruzuku kwa kaya za walengwa ili kuziwezesha kaya masikini kupata mahitaji ya msingi (Afya na Elimu) na fursa za kujiongezea kipato, kulinda rasilimali zao na kuweka akiba kwa ajili ya kujiletea maendeleo na hatimaye kujitoa katika umaskini

2.6   UHAULISHAJI WA FEDHA

Uhaulishaji fedha kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ulianza mwezi Agosti, 2015. Malipo kwa kaya masikini yanatolewa kwa miezi miwili miwili. Vile vile malipo kwa kaya masikini yanategemea utimizaji wa masharti ya afya na elimu kwa kaya husika,   Mpaka sasa malipo yametolewa kwa awamu kumi na moja ambazo ni mwezi Julai, 2015 – Januari, 2017 ambapo jumla ya Tshs. 1,092,868,000/=.

MAFANIKIO YALIYOANZA KUONEKANA

i)        Ruzuku imesaidia walengwa kumudu kupata mahitaji ya msingi kama vile chakula kwa milo mitatu, sare na vifaa vya shule. Hii imesaidia kuongezeka kwa mahudhurio ya wanafunzi shuleni.

ii)       Pia ruzuku imesaidia walengwa kujiunga na Mfuko wa Tiba kwa KAdi (TIKA) ambapo jumla ya walengwa 2464 waliunga na mfuko huo kwa mwaka 2016. Halmashauri imeendelea kuhamasisha walengwa kujiunga na TIKA mwaka huu 2017 jumla ya walengwa 936 wamejiunga na mfuko huu.   

iii)      Elimu ya lishe bora imekuwa ikitolewa kwa walengwa wanapohudhuria kliniki na wakati wa zoezi la malipo kwa walengwa hii itasaidia kupunguza hali ya udumavu kwa watoto.

iv)      Walengwa wameweza kuanzisha miradi midogo midogo kama vile ufugaji wa kuku, mbuzi wa maziwa, kondoo, sungura, bata, nguruwe na uuzaji wa maziwa ili kujingezea kipato.

v)       Pia baadhi ya walengwa wameweza kuboresha makazi yao.

vi)      Uanzishaji wa kikundi cha ufugaji wa kuku katika kata ya Ruaha na kikundi cha kuweka na kukopa kata ya Kitanzini ambapo walengwa wameanza kukopeshana.

vi)      Vile vile walengwa wamepata elimu ya ujasiriamali kupitia maafisa ugani waliopo katika kata. 

  •  

3.1 CHANGAMOTO

  • Mitaa 85 ambayo haijaingizwa kwenye Mpango wanaomba kuingizwa kwani kuna wahitaji katika mitaa hiyo.
  • Baadhi ya walengwa kutokuwa na makazi ya kudumu hivyo kusababisha fedha kurudishwa TASAF Makao Makuu kutokana na walengwa hao kutohudhuria siku ya malipo .
  • Mitaa mingi kupata fedha kidogo sana ya 1.5% hivyo kupelekea sehemu kubwa ya 8.5% kutumika kujazia 1.5% kwa mitaa hiyo wakati wa zoezi la malipo.
  • Baadhi ya wajumbe wa Kamati (CMC) kujiondoa katika Mpango bila taarifa kutokana na kulipwa posho kidogo, hivyo kusababisha tatizo siku za malipo.

Nawasilisha

Matangazo

  • TANGAZO LA KUONGEZWA MUDA WA KUCHUKUA FOMU YA UJENZI WA JENGO LA BIASHARA TEMBO BAR February 15, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA, 2023/2024 July 13, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI July 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 23, 2024
  • Soma zote

Habari za Hivi punde

  • PPP CENTRE YATOA MAFUNZO KWA WATAALAMU IRINGA MC

    April 04, 2025
  • ALUTE: "HAKIKISHENI MIRADI INAKAMILIKA KWA WAKATI NA KWA UBORA"

    December 21, 2024
  • UCHAGUZI HURU NA WA HAKI UNAHITAJI USHIRIKISHAJI - RC SERUKAMBA

    October 10, 2024
  • MSIGALA AWAONYA MAAFISA MAENDELEO KUJIHUSISHA NA MIKOPO HEWA

    October 05, 2024
  • Soma zote

Video

MEYA WA MANISPAA KUZIPIGANIA TIMU ZA MKOA KUPANDA DARAJA
More Videos

Viunganisho vya Haraka

  • National Examination Council of Tanzania
  • Watumishi Portal
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA,2023/2024
  • Sheria ndogo za Manispaa
  • Vivutio vya Utalii na Taarifda zake
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Tovuti Zinazofanana

  • Goverment Website
  • TAMISEMI
  • Iringa Region Website
  • IMtv Fahari ya Iringa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

Location Map

Wasiliana nasi

    Iringa Municipal Council

    Sanduku la Posta: 162

    Telephone: +255-2702647

    Mobile: 255-2702647

    Email: md@iringamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya usiri
    • Ukanusho
    • MMM
    • Ramani ya eneo
    • Huduma zetu

hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa